MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA VIWANJA KWA AJILI YA MATUMIZI MBALIMBALI VINAPATIKANA KATIKA WILAYA YA TANGANYIKA. VIWANJA HIVYO NI KWA AJILI YA MAKAZI, BIASHARA, MAKAZI NA BIASHARA, TAASISI, VIWANDA VIDOGO VIDOGO, MAHOTELI NA HUDUMA ZA KIJAMII. VIWANJA HIVYO VINAPATIKANA KATIKA MAENEO YA MAKAO MAKUU YA WILAYA (MAJALILA), KASEKESE, IKOLA NA KAREMA
BEI ELEKEZI YA VIWANJA HIVYO NI KUANZIA SHILINGI 700,000/= (MAJALILA), SHILINGI 559,500/= (IKOLA NA KAREMA) NA SHILINGI 342,000/= (KASEKESE). GHARAMA HIZI NI PAMOJA NA GHARAMA ZA HATI MILIKI.
KWA YEYOTE ATAKAYEHITAJI VIWANJA HIVYO ATATAKIWA KUJAZA FOMU YA MAOMBI NA KUITUMA AU KUIWASILISHA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA. GHARAMA ZA FOMU HIZO NI SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=) TU. FOMU ZINAPATIKANA OFISI ZA IDARA YA ARDHI NA MALIASILI - HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA .
PAKUA NAKALA HAPA: TANGAZO LA VIWANJA .pdf
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA ANUANI ZIFUATAZO:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA,
S.L.P 1,
MPANDA
SIMU NAMBA: 025 2820068
BARUA PEPE: ded@mpandadc.go.tz
Au tembelea website yetu: www.mpandadc.go.tz
IMETOLEWA NA:
Romuli Rojas John
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
NYOTE MNAKARIBISHWA
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.