Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani KATAVI ni miongoni mwa Halmashauri zinazoshiriki katika maonesho ya wakulima Nanenane ya Nyanda za juu kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya maonesho vya John Mwakangale Uyole Jijini Mbeya na ni moja ya Halmashauri inayofanya vizuri katika maonesho hayo kwa Halmashauri za mikoa ya nyanda za juu kusini kutokana na ubora za bidhaa zake na mambo yaliyopo katika banda la Halmashauri hiyo.
Halmashauri hiyo ambayo imekuwa inafanya vizuri katika maonesho hayo kwa miaka mitatu mfululizo, Katika maonesho ya mwaka huu imejipanga kutangaza kwa nguvu fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Halmashauri hiyo hasa eneo lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji lenye hekta 46, 000, kwa ajili ya uwekezaji na kuwashawishi wawekezaji wakawekeze katika eneo hilo sanjali na kutangaza vivutio vya utalii wa ndani kwa kutangaza eneo la utalii ikolojia la Luhafwe.
Akizindua Maonesho hayo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa amesisitiza suala la kutenga maeneo kwa ajili ya vijana waweze kujikita katika kilimo na suala la kuongeza thamani mazao ya wakulima ili kuongeza kipato na kumkomboa mkulima.
Kwa mantiki hiyo Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Kwa kutenga eneo la uwekezaji la Luhafwe pamoja na maeneo mengine ni jambo ambalo limepongezwa na kuzitaka Halmashauri nyingine zifanye kama Halmasauri ya Wilaya ya Mpanda.
Pia amewataka wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi wa Halmshauri za nyanda za juu kusini kushiriki katika maonesho ya utalii yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa kwa lengo la kufungua utalii kwa mikoa ya kusini na kuendeleza utalii wa Ndani ,ameeleza kwa kufanya hivyo wataweza kutangaza vivutio vilivyoko katika mikoa hiyo kama mbuga kubwa ya luaha, Hifadhi ya Katavi, Fukwe za ziwa Tanganyika na Nyasa na maeneo mengine ya Mikoa hiyo.
Maonesho ya wakulima NaneNane yanaendelea na yatafikia kilele chake Augusti Nane mwaka huu na kauli mbiu ya mwaka huu zalisha kwa tija ili kufikia uchumi wa kati.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.