Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kusimamia biashara ya Kaboni, ambayo imekuwa na manufaa kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Dkt Samia amesema kwamba Serikali itajipanga vizuri Zaidi ili kuongeza fedha zitokanazo na biashara hiyo, kwani kwa sasa Serikali haliridhishwi na faida inayotokana na mgao wa mauzo ya Kaboni Credit.
Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa 39, Vionogozi wa Jumuiya za Serikali za Mitaa-ALAT siku ya Machi 11 Jijini Dodoma.
“Wale wengine wa Tanganyika wana misitu wanauza Kaboni Credit, wanauza hewa ya ukaa fedha wanayoipata hata kama, Serikali haturidhishwi na wanacholipwa, bado tunafanyia kazi wanaweza kulipwa kitu kikubwa Zaidi” Mhe. Dkt Samia-Rais wa Tanzania
Sambamba na hilo ameagiza ofisi ya Makamu wa Rais kusimamia uingizaji wa misitu ya Tongwe Mashariki na Magharibi yenye ukubwa wa heka laki sita (600,000) kwenye biashara hii ili kuhakikisha eneo lile Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wanapata fedha wanayostaili kupata kwenye uuzaji wa kaboni credit.
“Hawa wanaouza wanatupunja sana, kwahiyo Tanganyika kabla ya kuendelea subirini kwanza Serikali iwasaidie kuipata fedha yenu” Mhe Dkt Samia, Rais wa Tanzania.
Biashara ya Kaboni imesaidia kwa kiasi kikubwa kunufaisha Wananchi wa vijiji nufaika moja kwa moja kutokana na miradi ya maendeleo itokanayo na faida ya biashara hii. Miongoni mwa faida hizo ni ujezi wa vituo vya afya, ujezi wa madarasa na shule, kutoa chakula bure mashuleni, kuajiri watumishi wa afya na walimu wa mkataba na kuwalipa mishahara, posho kwa Wenyeviti wa Vijiji.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.