Wakuu wa Idara ya Elimu, Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari wilayani Tanganyika wametakiwa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu upatikanaji wa chakula mashuleni ili kuondokana na tatizo la udumavu wilayani humo,
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Onesmo Buswelu alipokuwa akizungumza wakati wa kikao cha tathimini ya hali ya lishe katika wilaya hiyo,
Mheshimiwa Buswelu amesema kuwa ni lazima wahusika wote wa suala la lishe wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kampeni ya kuondokana na udumavu katika wilaya ya Tanganyika na Mkoa wa Katavi kwa ujumla inafanikiwa,
“Niwaombe wote wanaohusika katika suala la lishe katika wilaya yetu tuhakikishe tunatekeleza majukumu yetu kikamilifu ili tuweze kutokomeza kabisa changamoto ya udumavu katika wilaya yetu” amesema DC Buswelu,
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanganyika Bw. Lincoln Tamba amewataka wakuu wa shule kwa kushirikiana na kamati za shule kuhakikisha wanaunganisha nguvu ili upatikanaji wa vyakula kutoka kwa wazazi usiwe wa kusuasua,
“Wakuu wa shule shirikianeni na kamati zenu za shule ili muweze kuunganisha nguvu muwafikie wazazi wote ili waweze kuchangia vyakula kwa ajili ya watoto wao wanapokuwa mashuleni” amesema DAS Tamba,
Aidha, wahusika wote wa suala la lishe katika wilaya ya Tanganyika wametakiwa kuhakikisha suala la lishe bora linakuwa kipaumbele kikubwa ili kuweza kuyafikia malengo yaliyowekwa na Mkoa ya kuhakikisha changamoto ya udumavu inakuwa historia katika mkoa wa Katavi.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.